27 Agosti 2026 - 13:27
Qalibaf: Mahusiano ya Iran na China Hayahitaji Ruhusa ya Upande Wowote

Mwakilishi Maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya China, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema kuwa mahusiano kati ya Iran na China hayahitaji ruhusa kutoka kwa upande wowote.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwakilishi Maalumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya China, Mohammad Baqer Qalibaf, amesisitiza kuwa mahusiano kati ya Iran na China hayahitaji ruhusa kutoka kwa upande wowote.

Qalibaf amesema hayo kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake katika mtandao wa X siku ya Jumatano, akikaribisha msimamo wa China wa kupinga vikwazo anavyovitaja kuwa ni haramu vilivyowekwa dhidi ya Iran.

Amesema: “Tunakaribisha msimamo wa kimsingi wa China wa kukataa vikwazo visivyo halali vilivyowekwa dhidi ya Iran.”

Qalibaf ameongeza kuwa ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya Iran na China umejengwa juu ya misingi ya kuheshimiana, ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili, pamoja na mtazamo wa pamoja wa kujenga dunia yenye mfumo wa nguvu nyingi za kimataifa.

Kwa mujibu wa Qalibaf, misingi hiyo ndiyo inayounda msingi wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Tehran na Beijing, bila kuhitaji idhini kutoka kwa upande wa tatu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha